Nitatumia Google Tone vipi?
Ili kutuma URL kwa kutumia Google Tone:
- Ingia katika akaunti yako ya Google.
- Bofya kwenye aikoni ya Google Tone katika kivinjari chako cha Chrome ukiwa kwenye ukurasa wa wavuti unaotaka kutuma.
Kwa nini tutumie Google Tone?
Google Tone husaidia kompyuta kuwasiliana kama tunavyofanya—kwa kuzungumza. Ni kiendelezi cha kivinjari kinachoruhusu Chrome kutumia spika za kompyuta yako kutoa sauti maalum kwa maikrofoni za kompyuta nyingine ili kutambulisha kama URL.
Google Tone inafanya kazi vipi?
Google Tone huwasha maikrofoni ya kompyuta yako (kiendelezi kikiwa kimewashwa). Google Tone huhifadhi URL kwenye seva za Google kwa muda na hutumia spika na maikrofoni za kompyuta yako kuituma kwenye kompyuta zilizo karibu zilizounganishwa kwenye Intaneti. Kompyuta yoyote iliyo karibu ambayo pia imewekwa kiendelezi cha Google Tone na kiendelezi hicho kimewashwa inaweza kupokea arifa kutoka Google Tone. Arifa hiyo itaonyesha URL pamoja na jina na picha ya Wasifu unaotumia kwenye Google.
Ili kupokea URL ya Google Tone, Chrome inahitaji maikrofoni yako iwe imewashwa. Huenda Google Tone isifanye kazi katika mazingira yenye kelele, ikiwa kompyuta husika haziko karibu, ikiwa hakuna muunganisho thabiti wa Intaneti au kwenye kompyuta ambazo hazina maikrofoni au ikiwa maikrofoni iliyopo haiwezi kutambua sauti inayotumwa na Google Tone.
Google Tone inatumia data yangu vipi?
Google Tone hukusanya data ya matumizi bila kukutambulisha kama mtumiaji kwa mujibu wa Sera ya Faragha ya Google.
Nitaiwasha na kuizima vipi?
Ili kuwasha na kuzima Google Tone (ikiwemo maikrofoni), nenda kwenye mipangilio ya viendelezi vya Chrome.
Je, ni salama?
Google Tone hutuma URL pekee, kwa hivyo wapokeaji hawapati idhini ya moja kwa moja ya kufikia ukurasa ambao kwa kawaida wasingeweza kuufikia. Kwa mfano, ukituma URL yako ya kikasha cha Gmail, wapokeaji wanaobofya arifa kutoka Google Tone wataagizwa kuingia katika akaunti yao ya Gmail. Hata hivyo, matangazo kutoka Google Tone yameundwa ili yaonekane na umma, kwa hivyo ni vyema kutoyatumia kubadilishana maelezo ya siri.